Tuesday, February 13, 2018

MWENYEKITI WA CCM MSAAFU SONGEA MJINI AZIKWA LEO -SONGEA

PICHA-MPENDA MVULA.

Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Mapinduzi wilayani Songea ndugu Gerold Antoni Mhenga amezikwa leo na maelfu ya watu katika makaburi ya Bombambili Songea.


Marehemu Gerold Mhenga Alizaliwa Mwaka 1953 katika Kijiji cha Ndugaro Wiliayni Njombe Mkoa wa Njombe katika Parokia ya Uwemba.
Alianza shule ya Msingi Mwaka 1962 katika Kijiji cha Igoma mpaka darasa la Nne,Baada ya hapo alienda Midle School katika Shule ya Mtyang'imbole Mpaka Mwaka 1969.Mwaka 1972 Aliajiliwa Wizara ya Ujenzi(Mawasiliano)Songea baada ya apo aliacha kazi na kuendelea na Biashara.

Ibada ya Mazishi Ikiongozwa na Baba Naibu Askofu wa Jimbo la Songea Mjini .
Marehemu Gerold Antoni Mhenga alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Kiongozi na kufanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali,Mwaka 1998-2003 Alikuwa Kamanda wa Vijana wa CCM.
Mwaka 2002-2012 Alikuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wiliya na Mwaka 2012-2017 marehem Gerold Mhenga alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini na Baadae alistaafu Uongozi na kubakia kuwa mshauri wa Chama.
Mwili wa Marehemu Gerold Mhenga Ukielekea Makaburini

Mke wa Marehemu Gerold Mhenga akiweka taji.
Watoto wa Marehemu wakiweka shada la mauwa.

Marehemu Gerold Mhenga amefariki tarehe 10.02.2018 saa mbili Usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea na kuzikwa tarehe 13.02.2018 katika Makaburi ya Bombambili na ameacha mke na watoto Tisa,Wakiume watano(5)na Wakike wanne(4)na wajukuu kumi na tatu(13).
Umati wa watu walijitokeza nyumbani kwa Marehemu.
 Viongozi wa Chama na Serikali walikuwapo.
Watoto wa Marehemu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE AMEN.

No comments:

Post a Comment