Thursday, February 22, 2018

MBUNGE SONGEA MJINI ATOA VIFAA KTK KITUO CHA AFYA MJIMWEMA KWA NIABA YA RAIS.

Na- Mpenda Mvula-Songea

Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Mh.Dr.Damas Ndumbaro,ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vitanda 20 na Magodoro yake vyenye thamani ya sh. Milioni 18 kwa niaba ya Rais Dr.John Magufuli ikiwa moja ya utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa wakati wa Kampeni ya uchaguzi mkuu.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mh Dr.Ndumbaro alivitaja vifaa vingine vilivyotolewa katika kituo hicho cha Afya  kuwa ni Shuka 50 pamoja na vitanda vitano kwa ajili ya kujifungulia akina Mama wajawazito.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Manispaa ya Songea Dr.Mameritha Basike amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli kwa msaada wake alioutoa katika kusaidia kituo hicho cha Afya Mjimwema.

                                                         MWISHO.

No comments:

Post a Comment