Monday, November 14, 2016

SIKU YA KILELE CHA UGONJWA WA KISUKARI DUNIANI SONGEA ULIFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MANISPAA.

UIN- UJAMAA INTELLECTUALS
                   NETWORK 

Mwenyekiti Dr Geofrey L.Mdede Amesema:
Na Mpenda Mvula-Songea

 Siku ya kisukari duniani ni siku ambayo huadhimiswa ulimwengu mzima kila mwaka novemba 14.Lengo kubwa likiwa ni kuhamasisha ulimwengu uweze kutambua umuhimu wa huu ugonjwa ambao huambatana na kauli mbiu mbalimbali.Mfano Mwaka huu kauli mbiu ni"MACHO KWENYE KISUKSRI"Siku ya kisukari duniani ilianza kwa mara ya kwanza 1991 na Shirika la Kisukari Duniani(IDF)na baadae shirika la Afya duniani kuamua kuidhinisha rasmi kila mwaka baada ya kiwango cha ugonjwa huu unaongezeka kwa kasi.
 Mkuu wa wilaya ya Songea Paloleti Kamando Mgema akipima Kisukari katika kilele cha siku ya ugonjwa wa kisukari duniani iliofanyika katika viwanja vya bustani ya Manispaa.

Ujamaa Intellectuals Network ni nini? 
Mwenyekiti wa Mkoa Ruvuma Dr Geofrey L.Mdede anasema Ujamaa Intellectuals Network ni Asasi isiyo ya serikali ambayo ilianzishwa Machi 2013 na kupata usajili wa kudumu mwezi Septemba 29,2013.Ujamaa inahusisha vijana ambao waliokuwa vyuoni hadi mwaka 2010 ambao baada ya kuajiriwa na wengine kujiajiri katika nafasi mbalimbali walikuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali ambazo kuzitatua kwa namna moja au nyingine kwa mtu mmoja mmoja ilikuwa ni vigumu sana.Walikutana na kuamua kuanzisha Asasi hii ambayo itawaweka pamoja kama vijana.
 Wananchi walijitokeza kwa wingi kupimba Kisukari,uzito na Bp.

Lengo kubwa la Asasi hii ni kutoa elimu na majibu kwa jamii ya watanzania hasa Vijana ambao ndiyo nguvu kazi kubwa ya taifa katika nyanja mbalimbali kama uzalendo,kutoa elimu ya Afya,kutoa elimu ya utanzaji wa mazingira,kutoa elimu kuhusu rushwa na mambo mengine yanayoendana na hayo.
 Mwenyekiti wa UIN Dr.Geofrey Mdede akisoma Risala.


Baadhi ya wagonjwa wameshika mabango yenye kauli mbiu MACHO KWENYE SUKARI


 Baadhi ya wagonjwa wa kisukari walipata muda wa kuuliza maswali
Mkuu wa wilaya ya Songea ikipima uzito
Mkuu wa wilaya ya Songea Paloleti Kamando Mgema akipata maelezo kuhusu bima ya Afya (NHIF)
Watu wengi walijitokeza kupata vipimo katika viwanja vya bustani ya Manispaa upimaji ni bule.
PICHA ZAIDI NA MPENDAHABARI.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment