Monday, March 2, 2015

MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU MH.KAPT.JOHN KOMBA-SONGEA.

PICHA NA MPENDA MVULA-SONGEA
 Magari ya vyama vya siasa CCM na CHADEMA yalipaki uwanja wa ndege wa Songea kusubili mwili wa marehemu Mh.Kapt.John Komba.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mh.Mark Mwandosya na mwenyeji wake Said Thabit Mwambungu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakisubili mwili wa marehemu Mhe.Kapt. John Komba katika Uwanja wa ndege wa Songea.
 Umati wa watu waliojitokeza kuja kupokea mwili wa mpendwa wao Mh.Kapt.John Komba katika uwanja wa ndege wa Songea.
 Viongozi mbalimbali wakiwasili Mjini Songea.
 Ndege iliyobeba mwili wa marehemu Mh.Kapt.John Komba ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Songea.
 Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma  wakisubili mwili wa marehemu Mhe.Kapt.John Komba.
 Mke wa marehemu Mh.Kapt.John Komba akishuka uwanja wa ndege wa Songea.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akimfariji mke wa Marehemu Mh.Kapt.John Komba baada ya kuwasili Mjini Songea.
 Mwili wa marehemu Mh.Kapt.John Komba ukishuswa ndani ya ndege tayari kuelekea nyumbani kwao Lituhi Wilaya Nyasa kwa ajili ya mazishi.

 Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari la jeshi la wananchi JWTZ.


 Umati mkubwa wa watu walijitokeza katika uwanja wa michezo wa Majimaji kuja kutoa heshima zao za mwisho.
 Msafara uliongozwa na waendesha pikipiki maarufu kama yeboyebo.
 Mwili wa marehemu Mh.Kapt.John Komba Unaingia katika uwanja wa michezo wa Majimaji.


 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwasili katika uwanja wa Majimaji Songea.
 Mwili ulibebwa na Askari maarumu wa Bunge.
 Mke wa marehemu Mh.Kapt.Komba akiwasili katika uwanja wa michezo wa Majimaji ambapo watu wengi walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho.
 Baba Abate wa Abasia ya Hanga Thadei Mhagama aliongoza misa fupi iliyofanyika katika uwanja huo wa Majimaji.

 Katibu wa Mbunge akitowa historia ya Marehemu.
 Vyombo mbalimbali vya habari vikifatilia kwa makini.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu alimuelezea marehemu ni mtu mcheshi,mchapakazi ajui kukasilika,mpenda watu asa kwa jimbo lake la Nyasa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitowa heshima zake za mwisho.Mwili wa marehemu Mh.Kapt.John Komba umesafirishwa leo kuelekea kijijini kwake Lituhi Wilayani Nyasa kwa mazishi yatakayo fanyika apo kesho.

No comments:

Post a Comment