Tuesday, March 3, 2015

MAFUNZO YA KUPIKA CHAKULA CHA ASILI YALIOTOLEWA NA SHIRIKA LA PADI-SONGEA

PICHA NA MPENDA MVULA

Shirika lasilo la kiserikali  PADI Songea limetowa mafunzo ya kupika vyakula vyaa Asili kwa wazee wa Mjini Songea ili kuepukana ma magonjwa yasiyo ambukiza kama Kisukari,Shinikizo la damu,kansa na mengineyo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo mama Helen Majiba amesema watu wengi upata maladhi hayo kutokana nakula vyakula ovyo bila mpangilio,vyakula vingi vinavyopikwa uwekwa mafuta na chumvi nyingi usababisha kupata mgonjwa hayo.
Mkufunzi wa mafunzo wa vyakula vyaa Asili mama Helen Majiba akionyesha chakula cha Asili kilichopikwa tayari kwa kuliwa.
Ivi ni baadhi ya vyakula ambavyo bado avijapikwa.
Ivi ni haina ya viazi vinaitwa Magimbi
Mkufunzi mama Helen Majiba akiwafundisha baadhi ya wazee walioudhuria semina hiyo ya kupika vyakula vya Asili,hapa wakiandaa mboga aina ya Matembele.
Baadhi ya wazee walioudhulia semina wakimsikiliza kwa makini mkufunzi wa semina iyo mama Helen Majiba.

Mboga hii inaitwa matembele.
Baadhi ya wazee wanasemina wakijifunza kwa vitendo.
Chakula iki kipo tayari kwa kuliwa ni ndizi zilizo changanywa na mahalage mabichi na kalanga mbichi zilizosagwa,nyanya na vituguu ni chakula kizuri kwa watu wanye kisukari na shinikizo la damu.
Mboga ya majani inatakiwa ipikwe kwa Dr tano tu(5)
Mkufunzi wa mafunzo mama Helen Majiba akiwagawia chakula baadhi ya wazee  walioshiriki mafunzo hayo.

 Mkufunzi wa mapishi ya vyakula vya asili mama Helen Majiba akielekeza upikaji wa chakula cha asili kiitwacho Makande.
 Makande aya yamepikwa kwa mahindi mabichi,Soya,maboga,mboga ya majani mchicha,vitunguu,nyanya vyote vilichanganywa na kupikwa kwa muda wa saa moja.
 Mkufunzi msaidizi Dada Grace akila makande.
Wapiga picha nao walijaribu kuonja chakula hicho cha asili kiitwacho makande.

No comments:

Post a Comment