Saturday, April 27, 2013

WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KATIKA MANISPAA YA SONGEA


Pamoja na kuwepo kwa familia nyingi zinazoishi maisha ya kifahari katika maeneo mbalimbali  ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma bado kumeendelea kuwepo kwa wimbi kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi huku baadhi ya watoto hao wakieleza kuwa wanatumikishwa katika ajira mbali mbali ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na mamlaka mbali mbali pamoja na asasi zisizo za kiserikali zinazotetea haki za watoto.

 Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Songea na kuzungumza na baadhi ya watoto ambao walikutwa wakifanya biashara ya kuuza karanga ambazo walisema kuwa siyo zao bali wametumwa na waajiri wao kufanya biashara hiyo ambayo huifanya kutwa nzima na jioni wanalazimika kupeleka fedha kwa waajiri wao na walisema kuwa wamelazimika kujiingiza katika biashara hiyo kwa sababu ya umaskini wa kipato wa wazazi wao huku wengine wakiwa ni yatima ingawa wegine bado ni wanafunzi wa shule za msingi lakini uwezo wa wazazi kuwatimizia mahitaji yao ni mdogo.
  


 Wakati serikali pamoja na asasi zisizo za kiserikali zikiendelea kupiga kelele dhidi ya ajira kwa watoto lakini watoto hawa waliokutwa na mtandao huu walisema kuwa Afisa mmoja wa Manispaa ya Songea aliwataka ili waweze kuendelea kufanya biashara hiyo wanapaswa kuwa na sare mbayo mwajiri wao alilazimika kuilipia shilingi elfu tano na ndiyo hiyo walioivaa

Akizungumza kuhusiana na kauli hiyo ya watoto wanaofanya biashara hiyo kwa kutumikishwa na waajiri wa biashara hizo Afisa biashara wa Manispaa ya Songea Kelvin Challe kuwa Manispaa haitoi vibali wala leseni ya biashara yoyote kwa watoto bali watu wazima ndiyo hufika Manispaa kwa ajili ya kupata vibali vya biashara na baadhi yao huvitumia vibaya vibali hivyo kwa kwa kuwatumikisha watoto.

  Aidha alisema kuwa kunapaswa kuwepo kwa ushirikiano wa jamii nzima ili kudhibiti vitendo hivyo vya kuwatumikisha watoto kwenye ajira badala ya kuwaendeleza kielimu kwasababu urithi ulio bora kwa mtoto ni elimu.PICHA ZOTE NA MPENDA MVULA.

No comments:

Post a Comment