Mtoto yatima ambaye pia ni mremavu wa miguu na kupooza aitwaye Siwema Ngunga mwenye umri wa miaka minane mkazi wa mtaa wa Madizini mjini Songea mkoani Ruvuma amepata msaada wa kulipiwa ada ya Shule kwa Mwaka Mmoja ambayo ni Shilingi laki tatu na nusu (350,000) kutoka kwa mfanya biashara wa mjini songea mkoani ruvuma Bi Farida Mdaula pamoja na msaada wa kupata matibabu bure kutoka bima ya afya NHIF kwa muda wa mwaka mmoja. Picha na Mpenda Mvula.
Mtoto Siwema Ngunga akiwa amekaa kwenye Baiskeli yake ya Walemavu.
Mfanya Biashara Farida Mdaula akimkabidhi mtoto Siwema Ngunga pesa zilizochangwa na baadhi ya Wanawake waliojitokeza kwenye kilele cha siku ya Wanawake Duniani ambayo ililatibiwa na MM INTERTAIMENT katika ukumbi wa SWISS HOTEL iliyopo Songea Mjini.
Mfanyabiashara Bi Farida Mdaula akitokwa na machozi baada ya kupata historia ya mtoto Siwema Ngunga .
Meneja wa Bima ya Afya NHIF Abdiel E.Mkaro akimkabidhi fomu Siwema Ngunga kwa ajili ya kupatiwa matibabu bule kwa muda wa mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya MM INTERTAINMENT inayoshugulika na watoto waishio katika Mazingira magumu Marietha Msembele ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha habari cha CHANEL TEN akitowa maelezo juu ya mtoto Siwema Ngunga katika siku ya kilele cha siku ya wanawake duniani
Kutoka kushoto kwako ni Mkurungenzi wa blog ya mpendahabari.blogspot.com na wakwanza kulia kwako ni mwandishi wa habari wa chenel ten Jofrey Nilahi.
Mkurungenzi wa Ruvuma Habari Hamza Mashole akiwa katika picha ya pamoja na mtoto Siwema Ngunga.
No comments:
Post a Comment