Tuesday, February 17, 2015

MHE JENISTA MHAGAMA MBUNGE WA PERAMIHO AKIONGEA NA VIONGOZI WA UWT NA VIJANA -SONGEA

Na Mpenda Mvula,Songea.

MBUNGE wa jimbo la Peramiho ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu wa bunge ,Jenista Mhagama amewataka viongozi wa jumuhiya  za wazazi,Vijana na UWT kutoka chama cha  Mapinduzi (ccm) kuhakikisha wanafanya kazi ya kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuipigia kura katiba pendekezwa ili kutoa fursa ya upigaji kura kwa wananchi  wengi katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao.

Wito huo ameutoa jana wakati wa hafla fupi ya kumpongeza kupata nafasi mpya ya kuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu wa bunge iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa parokia ya Bombambili manispaa ya Songea  na kuhudhuriwa na viongozi wote wa jumuiya za chama hicho.

Alisema kuwa pamoja na mambo yote  ya maendeleo yanayofanywa na serikali inayongozwa na ccm kazi iliyobaki katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu nikuhakikisha wananchi wanajiandikisha kwenye daftari la kupigia kura pamoja na kuipigia kura katiba pendekezi.

Jenista alieleza zaidi kuwa kama viongozi wa jumuiya za chama hicho watasimama kidete kuhamasisha kwa wingi wananchi  kwenda kujiandikisha kwenye daftari hilo ,itatoa fursa kubwa kwa wapigakura kushiriki kazi hiyo na hatimaye kukifanya chama hicho kuendelea kushika dora .

“Ili chama chetu kiendelee kushika dora ni lazima viongozi wa chama toka kwenye jumuiya zenu kuinuka kwenda kufanya kazi ya kuhamasisha wananchi waende kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupigia kura na si vinginevyo kwani vitambulisho vya kupigia kura vya zamani havitatumika na msidanganywe na wanasiasa wa maji taka‘’alisema Waziri Jenista.

  Aidha Waziri  huyo licha ya kutoa maagizo hayo aligawa Baiskeri 19zenye thamani ya sh.2.2 kwa jumuiya ya wazazi ikiwa ni mwendelezo wa ahadi zake ambapo tayari alishagawa baiskeli hizo kwa jumuiya zingine za vijana na UWT kwa kila kata za jimbo lake .
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Songea vijijini Rajabu Uhonde akizungumza kwenye hafla hiyo kabla ya mgeni rasmi Jenista Mhagama kuzungumza na wanajumuiya hao alisema kuwa chama chake kimejipanga vizuri kuhakikisha maagizo yote yaliyotolewa  toka ngazi ya taifa yanafanyiwa kazi kwa utekelezaji na aliwaonya wale wote ambao wameonesha nia ya kutaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao wasubiri mpaka muda utakapofika vinginevyo watachukuliwa hatua za kinidhamu ndani ya chama.



Nao viongozi wa jumuiya hizo wakimshangilia Mbunge huyo walisema kuwa wao hawafikirii kuchagua mtu mwingine kwa kuwa aliopo anatosha kwa madai kuwa kawaletea maendeleo mbalimbali katika jimbo lao zikiwemo barabara ambazo zilikuwa hazipitiki katika vipindi vya nyuma ,elimu toka shule za sekondari 3 hadi kufikia 28,zahanati pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na kuongeza idadi ya walimu 349 walopo sasa.
      
MWISHO.

No comments:

Post a Comment