Tuesday, December 10, 2013

NMB RUVUMA YAADHIMISHA SIKUKUUU YA FAMILIA NCHINI.

PICHA MPENDA MVULA
UKUMBI-HERRITAGE COTTAGE

Wafanyakazi wa benki ya NMB wa matawi manne ya mkoa wa Ruvuma,wameadhimisha sikukuu ya Familia (NMB FAMILY DAY) kwa kushiriki michezo mbalimbali katika viwanja vya Seminari Peramiho nje kidogo na mji wa Songea.
Familia zilizo kutana katika sikukuu hiyo ni za wafanyakazi wa NMB  matawi ya Namtumbo,Mbinga,Litembo na Songea mjini ambapo pamoja na mambo mengine michezo waliyoshiriki ni mazoezi ya viungo,kuvuta kamba,mpira wa miguu,Basketball na kufukuza kuku.
Lakini pia pamoja na Familia hizo kutembelea mabwawa ya samaki yanayomilikiwa na Seminari kuu Peramiho,wakashiriki chakula cha pamoja katika Hotel ya Herritage Cottage,kucheza muziki pamoja na kupeana zawadi mbalimbali.

KAULI MBIU YA NMB FAMILY DAY MWAKA HUU <FAMILA KWANZA.<

1 comment: