Na Mpenda Mvula,Songea.
WATU saba wanaodaiwa kuunda mtandao wa
kigaidi Songea mkoani Ruvuma wameshakamatwa na muda wowote kuanzia sasa
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowabili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana
kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa watuhumiwa hao
ambao majina yao yamehifadhiwa wanadaiwa kuhusika na matukio matatu tofauti ya
urushwaji na utegaji wa mabomu ya kienyeji.
Alifafanuwa kuwa tukio la kwanza lilitokea
Septemba 16 mwaka jana majira ya saa 1.30 jioni huko katika eneo la Misufini
kikundi hicho kinachojihusisha na ugaidi kiliwarushia Askari polisi waliokuwa
doria bomu la kienyeji la kurushwa ambalo liliwasababishia askari watatu kujeruhiwa.
Alisema kuwa katika tukio lingine ambalo lilitokea
Oktoba 27 mwaka jana majira ya saa 10 jioni lilichimbiwa ardhini bomu katika
eneo la Mshangano ambalo hutumiwa kama kituo cha ukaguzi wa magari yanayotoka
na kuingia Songea mjini na askari wa kikosi cha usalama barabarani kando kando
mwa Barabara inayotoka Songea kwenda Njombe kwa lengo la kuwalipua askari wa
kikosi hicho.
Kamanda Msikhela alieleza zaidi kuwa pia
kabla hawajatimiza hazma hiyo askari wa usalama barabarani waliokuwa kwenye
eneo hilo waliligunduwa bomu hilo likiwa limechimbiwa ardhini na jeshi la
polisi kwa kushilikiana na jeshi la wananchi (JWTZ) baada ya kupata taarifa
hiyo walifika kwenye eneo la tukio na waliweza kuliteguwa bila kuleta madhara.
Alilitaja tukio lingine la tatu kuwa
lilitokea Disemba 25 mwaka jana majira ya 1.30 usiku katika eneo la Majengo
Kotazi kikundi hicho cha ugaidi pia kilidhamilia kuwarushia bomu askari
waliokuwa wanafanya doria ambapo mtu mmoja kutoka katika kikundi hicho
alijaribu kuwarushia bomu askari hao na kabla hajarirusha lilimlipukia yeye mwenyewe
na kufariki Dunia papo hapo na kusababisha askari polisa wawili
kujeruhiwa
vibaya.
Alieleza zaidi kuwa timu ya upelelezi toka
ndani ya jeshi la Polisi kwakushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama vimeweza kubaini eneo linalotumika kwa mafunzo ya kigaidi na kikundi
hicho na kwamba mpaka sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo na wanatarajia
kupanda mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment