Tuesday, February 17, 2015

KITUO CHA MAFUTA TUNDURU CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI.

Na Mpenda Mvula,Songea.

WATU 3 wanaozaniwa kuwa ni majambazi hambao walikuwa na siraha inayodaiwa kuwa ni SMG pamoja na mapanga huku wakiwa wamejifunga vitambaa vyeusi husoni walivamia kituo cha mafuta cha Jamuhuli Petrol felling station kilichopa katika eno la mtaa wa kalanje  mjini Tunduru mkoani Ruvuma na kupola fedha taslim shilingi million 7 pamoja na simu moja ya mkononi yenye thamani ya shilingi laki tisa na elfu themanini kasha walikimbia na kutokomea kusiko julikana
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3 na nusu usiku huko katika kituo cha kuuza mafuta ya vyombo vya moto cha Jamuhuli Petrol felling station cha mjini humo.

Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio watu 3 wasiofahamika majina yao wala sura zao wakiwa na bunduki aina ya SMG huku wakiwa na mapanga walivamia kituo hicho cha mafuta na kuwatishia kuwapiga Risasi wafanyakazi wakituo hicho huku wakidai watoe fedha walizokuwa nazo na baadaye walifanikiwa kunyang’anya fedha  shilling million 7 pamoja na simu moja ya mkononi Sumsang Gallaxy huku wamewawekwa chini ya ulizi mkali wafanyakazi wa kituo cha mafuta akiwemo Nasri Salum(27) mwenye asiri ya kiarabu ambaye alikuwa anakamilisha mahesabu ya mauzo ya siku hiyo.

Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa awali majambazi hao walifika katika kituo hicho cha mafuta mapema kama wateja wengine wakiwa na gari ambalo namba zake za usajili hazikuweza kufahamika mara moja na baada ya kuhudumiwa walienda kulipa pesa dirishani ghafla walitoa bunduki 2 na kufyatua risasi mbili hewani kisha kutoa mapanga na kuwatishia kuwauwa wafanyakazi wa kituo hicho huku majambazi hao wakidai watoe fedha zilizokuwepo kwa wakati huo kwenye kituo hicho.

Alisema kuwa majambazi hao walifanikiwa kupora kiasi hicho cha fedha kisha walikimbia na kutokomea kusiko julikana ndipo baada ya hapo wafanyakazi walikimbilia kituo kikuu cha polisi kutoa taarifa ya tukio hilo.

Kamanda Msikhela baada ya tukio hilo kulipotiwa polisi askali polisi walikwenda kwenye eneo la tukio  na kulifanyia uchunguzi wa kipolisi ambapo waligundua maganda mawili ya lisasi yaliyotumika na walipoyafanyia uchunguzi ilibainika kuwa ni risasi ya bunduki aina ya SMG.

Hata hivyo kamanda Msikhela alisema kuwa Jeshi la Polisi mkoni  humo linaendesha msako mkali wa kuwasaka majambazi hao na amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuona umuhimu wa kutoa ushilikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa zinazoweza kufanikisha kuwakamata majambazi hao.

Mwisho


  

No comments:

Post a Comment