Tuesday, March 18, 2014

UWARIBIFU WA BARABARA WILAYA YA MBINGA.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akikagua eneo lililofanyiwa uharibifu na wachimbaji wadogo wadodo wa madini waliopo katika kijiji cha Mkako wilayani Mbinga ambapo wameweza pia kuvamia eneo linalomilikiwa na jeshi la magereza Tanzania gereza la kilimo la Kitai.

 Wachimbaji hao pia wamefanya uharibifu kwenye eneo la barabara kuu ya Songea -Mbinga jambo ambalo linahatarisha usalama wa raia ambao wanatumia barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kugharimu zaidi ya sh. bilioni 78 .
 Hili ni moja ya mashimo ambalo limechimbwa na wachimbaji wadogowadogo wa madini wa eneo la Kitai na kuachwa bila kufukiwa huku serikali na taasisi binafsi zikiimiza utunzaji wa mazingira .swali kwa serikali na wizara husika je vita hii ya utunzaji wa mazingira itafanikiwa? Je elimu ya utunzaji wa mazingira imetolewa vya kutosha kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini? kazi kwako msomaji.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bi. Senyi Ngaga  mwenye shati jekundu wakiendelea na ukaguzi wa maeneo hayo ya Kitai waliopo nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa.

No comments:

Post a Comment