Thursday, January 9, 2014

WANANCHI NA VIONGOZI WA MKOA WA RUVUMA WAMETAKIWA KUDUMISHA AMANI.

Na Mpenda Mvula.
Wananchi na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kudumisha Amani na kuacha maneno ya uzushi katika kipindi cha Mwaka huu wa 2014 ambapo kuna mchakato wa kupata Katiba mpya na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu wakati akizungumza na Viongozi,Wananchi na Wabunge wakiwemo wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma kwenye Hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Songea Club.

Amewataka Viongozi wa siasa Mkoani humo kufanya siasa za amani na kutoeneza maneno ya uzushi,Amesisitiza kuwa amani iliyoko Mkoani Ruvuma siyo ya kuchezea na kwamba ni jukumu la Wananchi wote kuidumisha.
Hafla ilifunguliwa kwa sara na Padre Danstan Mbano.
Baadhi ya Viongozi waliudhuria.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiwa na baadhi ya viongozi wa Kidini
Baadha ya viongozi wakisikiliza kwa makini .
Kwaito kama kawaida.
PICHA NA MPENDA MVULA.0755-556736/0716-162889 SONGEA.

No comments:

Post a Comment