27 Februari,2013
Mheshimiwa Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka Lichinga Msumbiji.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB) akisalimiana na Wazee wa Jadi.
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Akivalishwa Vazi la kijadi na Chifu Xsavery Emmanuel Zuru.
Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na Meya wa Lichinga Nchini Msumbiji.
Mgeni rasmi Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki(MB) Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea ndugu Barthazary Nyamusya.
Msafara kutoka katika Ukumbi wa Songea Club kuelekea katika Makaburi ya Mashujaa yaliopo Mahenge Songea Mjini.
Mwanahabari Gerson Msigwa wa TBC Akiwa kazini.
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akiweka Ngao mahala walipo nyongewa mashujaa hao.
Chifu Xsavery Emmanuel Zuru ikielekea kuweka silaha za jadi mahala walipo nyongwa Mashujaa hao.
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Waziri wa Maliasili na Utalii akielekea kuweka Ngao na Mkuki Mahala wilipozikwa Mashujaa hao.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.
Chifu Xsavery Emmanuel Zuru.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu.
Ngoma ya Wazee wa Kingoni inaitwa LIGIHU.
Mheshimiwa Balozi Hamisi Kagasheki(MB) Waziri wa Maliasili na Utalii.
Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea Barthazary Nyamusya akitoa Historia kwa mgeni rasmi.
Picha na Mpenda Mvula.
SIKU ya kumbukizi ya maadhimisho ya mashujaa wa vita ya Maji maji imefanyika mjini Songea mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasmi Waziri wa Mali asili na utalii Dkt.Hamis Kagasheki akiitaka jamii nchini kuenzi harakati hizo zilizofanywa na mababu wa taifa hili katika kupinga utawala wa kikoloni.
Aidha alisema kuwa katika chumba cha historia ya makumbusho hayo ameshuhudia kuwepo kwa taarifa za mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama Mkomanile ambaye alishiriki katika harakati hizo za mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni hivyo ni ishara kuwa akina mama nao walishiriki kikamilifu katika mapambano hayo dhidi ya ukoloni ambapo kwa upande wa Tnganyika ilikuwa ni Vita ya Maji maji ,na kwa upande wa Kenya ilikuwa ni Mau mau na vyote vilikuwa ni chanzo cha vuguvugu la ukombozi wa bara la Afrika.
Aidha alitoa wito kwa wadau wa utafiti watafiti zaidi habari za mwanamke huyo ili nazo ziweze kuingizwa kwenye historia ya kumbukizi hiyo ya vita ya Maji maji ambayo pia ilikuwa ni chachu ya ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.
Maadhimisho hayo ambayo yalihudhuriwa na wakuu wa mikoa kadhaa akiwemo Joel Bendera(Morogoro),Dkt.Rehema Nchimbi(Dodoma) na Kapteni Mstafu Asery Msangi(Njombe) yalitanguliwa na uwekeja wa silaha za jadi kwenye makaburi ya mashujaa hao pamoja na dua za viongozi wa dini kutoka madhehebu mbali mbali ambao katika dua zao waliiomba jamii nchini kudumisha amani,upendo na utulivu na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuliingiza taifa katika machafuko yakiwemo ya udini au ukabila.
No comments:
Post a Comment